Posts

Tazama ajali ilivyokwamisha ndoto za kijana huyu

Image
Na Adrian Mgaya. Inasikitisha kwa kweli Ketson John, aligongwa na pikipiki ikamkata mguu na kumtupia kwenye mataluma ya reli, kabla hata hajainuka treni ikampitia na kumkata mguu uliosalia... Mtazame hapa kupata undani wa maisha yake.

KWANINI SHERIA HAIWABANI WANAOKAA VITI VYA NYUMA KUFUNGA MKANDA?

Na Adrian mgaya Shirika la afya duniani linataja viashiria vikuu vya ajali za barabarani kuwa ni kutokuvaa kofia ngumu kwa waendesha pikipiki, mwendokasi usiofaa, matumizi ya vilevi kwa madereva, kutotumia vizuizi vya watoto na kutofunga mkanda wa usalama katika vyombo vya usafiri. Pamoja na viashiria hivi kutajwa kuwa ni vyanzo vikuu vya ajali na kuongezeka kwa madhara ya ajali za barabarani bado sheria mama ya usalama barabarani nchini Tanzania, haijagusia kiundani mambo haya ili kuendana na matakwa ya umoja wa mataifa kupitia shirika la afya duniani. Ambapo wanapendekeza sheria madhubuti zitasaidia kupunguza vifo na majeruhi wa ajali katika barabara zetu. Edda sanga, Mkurugenzi mtendaji wa TAMWA anasema "Umoja wa mataifa na shirika la afya duniani wanakiri kwamba sheria madhubuti zinahitajika katika kupunguza idadi ya watu wanaofariki katika barabara zetu. Tanzania lazima tuwe na sheria kali za usalama barabarani kukomesha hali hii” Sheria ya usalama barabarani ya m...

"WANASIASA WA NAWAPA KIBURI WAENDESHA BODABODA MBEYA"

Image
Na Adrian Mgaya Baadhi ya madereva wa pikipiki na bajaj mkoani Mbeya ambao wengi wao wana umri chini ya miaka 35, wapo katika hatari ya kupata madhara yatokanayo na athari za ajali za barabarani kutokana na kuwa wakaidi kwa mamlaka zinazosimamia usalama barabarani. Butusyo Akimu Mwombelo ambaye ni mkuu wa kikosio cha usalama barabarani mkoa wa Mbeya anasema, ongezeko kubwa la ajali za barabarani linachochewa na madereva wa pikipiki na bajaj. Hata hivyo juhudi za kupambana na hali hiyo zina vikwazo vingi kutokana na mwingiliano na mambo ya siasa. Tazama video hii kufahamu zaidi.
Image
Sanamu ya Askari Bonge la kivutio . by Adrian Mgaya. Macho hayana pazia ukweli huu unajidhihirisha pale ambapo umekatisha katikati ya jiji la Dar es salaam, achilia mbali shughuli ambazo unaweza ukawa nazo punde upitapo maeneo hayo hutoacha kutupia jicho vitu vilivyopo eneo hilo. Moja kati ya vitu ambavyo huvutia macho ya wakazi wengi pamoja na wageni wanaotembelea jiji la Dar es salaam ni sanamu kongwe ambapo ni nadra kuona mtu akatizaye eneo hilo kumuona akiacha kutupia jicho sanamu hilo. Licha ya pilika pilika zisizoisha zinazoendelea katika eneo linalojulikana kama posta ambapo sanamu ammbalo hutambulika kama sanamu la askari inapatiakana huwezi kukosa kuona baadhi ya watu wakishangaa na wengine hata kupiga picha (selfie) eneo lilipo sanamu hilo. Eneo lilipowekwa sanamu hilo la askari ni eneo la katikati ya barabara lililozungushiwa bustani ndogo ya maua inayoongeza ladha ya mvuto wa sanamu hilo, kuwepo kwa sanamu hilo eneo la katikati ya barabara kunatoa fursa ya ida...