Posts

Showing posts from January, 2016
Image
Sanamu ya Askari Bonge la kivutio . by Adrian Mgaya. Macho hayana pazia ukweli huu unajidhihirisha pale ambapo umekatisha katikati ya jiji la Dar es salaam, achilia mbali shughuli ambazo unaweza ukawa nazo punde upitapo maeneo hayo hutoacha kutupia jicho vitu vilivyopo eneo hilo. Moja kati ya vitu ambavyo huvutia macho ya wakazi wengi pamoja na wageni wanaotembelea jiji la Dar es salaam ni sanamu kongwe ambapo ni nadra kuona mtu akatizaye eneo hilo kumuona akiacha kutupia jicho sanamu hilo. Licha ya pilika pilika zisizoisha zinazoendelea katika eneo linalojulikana kama posta ambapo sanamu ammbalo hutambulika kama sanamu la askari inapatiakana huwezi kukosa kuona baadhi ya watu wakishangaa na wengine hata kupiga picha (selfie) eneo lilipo sanamu hilo. Eneo lilipowekwa sanamu hilo la askari ni eneo la katikati ya barabara lililozungushiwa bustani ndogo ya maua inayoongeza ladha ya mvuto wa sanamu hilo, kuwepo kwa sanamu hilo eneo la katikati ya barabara kunatoa fursa ya ida...