Sanamu ya Askari Bonge la kivutio.

by Adrian Mgaya.

Macho hayana pazia ukweli huu unajidhihirisha pale ambapo umekatisha katikati ya jiji la Dar es salaam, achilia mbali shughuli ambazo unaweza ukawa nazo punde upitapo maeneo hayo hutoacha kutupia jicho vitu vilivyopo eneo hilo.
Moja kati ya vitu ambavyo huvutia macho ya wakazi wengi pamoja na wageni wanaotembelea jiji la Dar es salaam ni sanamu kongwe ambapo ni nadra kuona mtu akatizaye eneo hilo kumuona akiacha kutupia jicho sanamu hilo.
Licha ya pilika pilika zisizoisha zinazoendelea katika eneo linalojulikana kama posta ambapo sanamu ammbalo hutambulika kama sanamu la askari inapatiakana huwezi kukosa kuona baadhi ya watu wakishangaa na wengine hata kupiga picha (selfie) eneo lilipo sanamu hilo.

Eneo lilipowekwa sanamu hilo la askari ni eneo la katikati ya barabara lililozungushiwa bustani ndogo ya maua inayoongeza ladha ya mvuto wa sanamu hilo, kuwepo kwa sanamu hilo eneo la katikati ya barabara kunatoa fursa ya idadi kubwa ya watu kujionea sanamu hilo bila kutoa gharama ya aina yoyote.

Ukiisogelea kwa ukaribu sanamu hiyo utagundua kuwa limepambwa na sare za jeshi zilizotumika katika jeshi la kikoloni enzi za waingereza (K A R). shati la mikono mifupi pamoja na kaptula vinaongeza umaridadi wa sanamu hilo. Miguuni sanamu hilo limevalia viatu imara pamoja na soksi zilizoishia chini kidogo ya magoti.
Sanamu la askari limeangalia upande ilipo bandari ya bahari ya Hindi, huku mgongoni kukiwa na begi na mkononi askari huyo anaonekana ameshika bunduki iliyochomekwa singe mbele kwa ukakamavu hii ikiwa ni ishara kwamba askari huyo yuko tayari kwa mapambano muda wowote ule.
Ukiongea na wengi wa wazee pamoja na wenyeji wa jiji la Dar es salaam watakupa sababu kemkem zinazovutia kuhusiana na sanamu hilo aliyebatizwa jina la Bismin swali ambalo wengi hujiuliza ni kwanini sanamu  huyo amegeukia upande wa ilipo bahari ya Hind na si sehemu nyingine?
Jibu utakalokutana nalo lazima likushangaze wenyeji hudai kuwa sanamu hilo limeangalia katika njia waliyotumia wajerumani kuingia Tanganyika na njia hiyo hiyo ndiyo iliyotumika kuwafukuza wajerumani kurejea kwa ambapo kazi hiyo ilifanywa na waingereza kwa ushirikiano wa karibu na wenyeji ambao ndio wazawa.
Hii ilikuwa kama ni ishara ya ushindi kwa waingereza ambao walikuwa wakipambana na wajerumani katika vita kuu ya kwanza ya dunia, hivyo kumwondoa mjerumani na kushikiria ngome yake ilikuwa ni moja ya mafanikio makubwa kwa waingereza.
Kitu kikubwa kinachovutia katika sanamu hilo ni maneno yaliyopo katika sanamu hilo ambapo huwezi kuyatambua maneno hayo kama yapo mpaka usogelee kwa ukaribu ambapo utagundua ujumbe ulioandikwa hapo uliandikwa na mtu makini mwenye ujuzi wa lugha na anayepangilia vizuri maneno yake.
"Huu ni ukumbusho wa askari Waafrika wenyeji waliopigana katika Vita Kuu na ni ukumbusho pia kwa wapagazi ambao walikuwa miguu na mikono ya majeshi. Ni ukumbusho pia kwa watu wote waliotumika wakafa kwa ajili ya mfalme na nchi yao katika Afrika ya Mashariki kwenye Vita Kkuu toka mwaka 1914 mpaka 1918 . Ukipigania nchi yako ujapo umekufa watoto wako watalikumbuka jina lako." Haya ni baadhi ya maneno yanayopatikana eneo liliposimikwa sanamu hilo.
Vilevile kuna maneno mengine yasemayo “ukiipigania nchi yako ujapo umekufa watoto wako watalikumbuka jina lako” hii ni ishara tosha kuonesha mashujaa walijitoa kwa moyo mmoja kupigania nchi yao na ndio maana sanamu hilo likawa pale mpaka sasa wapiganaji wanakumbukwa na kuenziwa kupitia sanamu hilo.
Ukipipitia mapitio mbalimbali ya kihistoria kuhusiana na sanamu hilo utapata kujua kwamba Mahali ilipowekwa sanamu hii paliwahi kuwekwa sanamu ya meja Hermann von Wissmann aliyekuwa gavana wa kwanza wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani na sanamu hii ilibomolewa na Waingereza walipoteka mji katika mwaka 1916.
Upande wa kushoto na kulia wa sanamu hilo panaonekana picha ambazo zinaongeza mvuto wa sanamu hilo.
Picha ya kwanza wanaonekana askari waliopo katika mapambano kiongozi wao anaonekana kama akitoa maelekezo ambayo yatawasaidia kumshinda adui, askari wengine wawili wakiwa wamekaa mkao wa kuweka tayali kombora na askari wengine wanne wakiwa wamekamata bunduki zao kwa ukakamavu tayari kwa mapambano huku nyuma yao akiwepo mpagazi aliyebeba mzigo begani.
Picha ya upande mwingine inawaonesha wapagazi ambao wanaonekana kubeba mizigo mizito kwani wanatembea kwa kusaidiwa na fimbo hii ikiwa ni ishara wametembea umbali mrefu na wana mizigo mizito. Idadi ya wapagazi hao ni saba huku wakionekana wakisindikizwa na askari aliyebeba bunduki kama inavyoonekana katika picha.
Hakika sifa za sanamu hilo ni nyingi zisizoweza kumalizika hata kwa kuandika zaidi ya makala moja. Wananchi wanatakiwa kutunza na kulithamini sanamu hilo. Kama ambavyo tunaona katika filamu nyingi za kitanzania sanamu hilo lokitumika kuutambulisha mji wa Dar es salaam katika filamu.
Endapo sanamu hilo lisipotunzwa tunaweza kupoteza sanamu hilo katika historia ya tanzania miaka ya nyuma iliwahi kuripotiwa katika mtandao wa jamiiforum kuwa sanamu hilo lilivamiwa na kuharibiwa na watu wasiojulikana, habari kama hiyo ililipotiwa katika blog ya Issamichuzi Mamlaka husika inapaswa kusimamia kwa umakini sanamu hilo ili pasitokee aina yoyote ya uharibifu.
Wageni mbalimbali wanaonekana kuishangaa sanamu hilo lakini kuna viashiria ambavyo ni tabia mbaya ambayo tunajaribu kuiendekeza watanzania ikiwa ni uchafu ambapo iliwahi kuripotiwa katika mtandao wa jamiiforum lakini kilio kikasikika na sanamu hilo lilifanyiwa usafi wa hali ya juu siku ya desemba 9 siku iliyotangazwa kuwa siku ya usafi ambapo katika blog ya tanzaniatoday tukio la kufanyiwa usafi sanamu hilo lilipotiwa.

Ni wazi kuwa miji mikubwa huwa na kiashiria kinachoutambulisha mji huo kama ilivyo kwa sanamu ya yesu jijini Rio De Jeneiro Brazil, daraja la London Uingereza na mnara wa Paris ufaransa.

Comments

Popular posts from this blog

KWANINI SHERIA HAIWABANI WANAOKAA VITI VYA NYUMA KUFUNGA MKANDA?