Na Adrian mgaya Shirika la afya duniani linataja viashiria vikuu vya ajali za barabarani kuwa ni kutokuvaa kofia ngumu kwa waendesha pikipiki, mwendokasi usiofaa, matumizi ya vilevi kwa madereva, kutotumia vizuizi vya watoto na kutofunga mkanda wa usalama katika vyombo vya usafiri. Pamoja na viashiria hivi kutajwa kuwa ni vyanzo vikuu vya ajali na kuongezeka kwa madhara ya ajali za barabarani bado sheria mama ya usalama barabarani nchini Tanzania, haijagusia kiundani mambo haya ili kuendana na matakwa ya umoja wa mataifa kupitia shirika la afya duniani. Ambapo wanapendekeza sheria madhubuti zitasaidia kupunguza vifo na majeruhi wa ajali katika barabara zetu. Edda sanga, Mkurugenzi mtendaji wa TAMWA anasema "Umoja wa mataifa na shirika la afya duniani wanakiri kwamba sheria madhubuti zinahitajika katika kupunguza idadi ya watu wanaofariki katika barabara zetu. Tanzania lazima tuwe na sheria kali za usalama barabarani kukomesha hali hii” Sheria ya usalama barabarani ya m...