"WANASIASA WA NAWAPA KIBURI WAENDESHA BODABODA MBEYA"
Na Adrian Mgaya Baadhi ya madereva wa pikipiki na bajaj mkoani Mbeya ambao wengi wao wana umri chini ya miaka 35, wapo katika hatari ya kupata madhara yatokanayo na athari za ajali za barabarani kutokana na kuwa wakaidi kwa mamlaka zinazosimamia usalama barabarani. Butusyo Akimu Mwombelo ambaye ni mkuu wa kikosio cha usalama barabarani mkoa wa Mbeya anasema, ongezeko kubwa la ajali za barabarani linachochewa na madereva wa pikipiki na bajaj. Hata hivyo juhudi za kupambana na hali hiyo zina vikwazo vingi kutokana na mwingiliano na mambo ya siasa. Tazama video hii kufahamu zaidi.